Tunafanya kazi njiani, majumbani na shuleni ili wasichana na wanawake wawe salama dhidi ya rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia.
Safari Salama Bila Rushwa ya Ngono
Kampeni kuu ya WAJIKI ilianza mwaka 2018. Tunatoa mafunzo kwa madereva wa bodaboda, bajaji na daladala, makondakta na viongozi wa vituo ili wawe walinzi wa wasichana na wanawake wanaowasafirisha.
Awamu ya sita ilizinduliwa Bunju A na inaendelea katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, kwa ushirikiano na vyama vya madereva, polisi wa usalama barabarani na LATRA, kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania Trust.
Timu zetu hupita nyumba kwa nyumba kuzungumza na familia kuhusu ukatili wa kijinsia, rushwa ya ngono na namna ya kutoa taarifa. Elimu hii inawafikia wazazi na walezi pale walipo.
Tunaanzisha na kuimarisha klabu za kupinga rushwa ya ngono katika shule za msingi na sekondari. Watoto wanajifunza haki zao na wanatoa taarifa za ukatili wanaofanyiwa majumbani na mitaani. Zaidi ya watoto 4,300 wamefikiwa.
Kuwa sehemu ya safari salama
Changia kupitia Mixx by Yas na uwasaidie wasichana kufika shuleni na kazini salama.