Kampeni ya WAJIKI tangu 2018

Safari Salama Bila Rushwa ya Ngono Inawezekana

Tunawawezesha madereva wa bodaboda, bajaji na daladala kuwa walinzi wa wasichana na wanawake njiani, shuleni na kazini.

Matokeo ya kampeni

Tangu 2018, maelfu ya madereva na wanafunzi wamejiunga na safari salama. Takwimu hadi Desemba 2022.

6,000+

Madereva wa bodaboda wamefikiwa

4,325

Watoto na wanafunzi wamepata elimu

459

Watu wazima wamefikiwa moja kwa moja

3

Wilaya: Kinondoni, Ilala na Temeke

Tatizo na suluhisho

Rushwa ya ngono huanzia njiani

Wasichana wengi hukutana na vishawishi na unyanyasaji wanaposafiri kwenda shule au kazini. Madereva wa vyombo vya usafiri ndio watu wa karibu zaidi nao kila siku, hivyo wanaweza kuwa sehemu ya suluhisho.

Jinsi kampeni inavyofanya kazi

1

Tunawafundisha madereva

Mafunzo kwa vijiwe vya bodaboda, bajaji na daladala kuhusu rushwa ya ngono, sheria na haki za mtoto.

2

Wanakuwa mabalozi

Madereva waliopata mafunzo huwaelimisha wenzao na kuwalinda wasichana wanaowasafirisha.

3

Jamii inatoa taarifa

Watoto, wazazi na walimu wanajua namna ya kuripoti ukatili kupitia klabu za shule na kampeni ya Door to Door.

Tazama makala ya Safari Salama

Sikia moja kwa moja kutoka kwa madereva, wanafunzi na jamii jinsi kampeni ya Safari Salama Bila Rushwa ya Ngono Inawezekana inavyobadilisha maisha jijini Dar es Salaam.

“Sisi madereva bodaboda tunapaza sauti kupinga na kukemea rushwa ya ngono. Tumlinde mtoto wa kike na tumsaidie ili atimize ndoto zake.”
Sauti ya Bodaboda, mabalozi wa Safari Salama

Programu zetu

Safari Salama Bila Rushwa ya Ngono

Kampeni kuu ya WAJIKI pamoja na wadau wa usafirishaji jijini Dar es Salaam.

Fuatilia kampeni

Door to Door

Elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia nyumba kwa nyumba, kwa familia na jamii.

Soma habari

Elimu kwa Watoto

Klabu za shule za kupinga rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa msingi na sekondari.

Angalia programu

Habari mpya

Tunaoshirikiana nao

Kuwa sehemu ya safari salama

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp kupata maelekezo rasmi ya kuchangia, na uwasaidie wasichana kufika shuleni na kazini salama.